90أُولٰئِكَ الَّذينَ هَدَى اللَّهُ ۖ فَبِهُداهُمُ اقتَدِه ۗ قُل لا أَسأَلُكُم عَلَيهِ أَجرًا ۖ إِن هُوَ إِلّا ذِكرىٰ لِلعالَمينَ Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewahidi. Basi fuata hidaya yao. Sema: Mimi sikuombeni ujira. Haya hayakuwa ila ni mawaidha kwa walimwengu wote.