37إِن تَحرِص عَلىٰ هُداهُم فَإِنَّ اللَّهَ لا يَهدي مَن يُضِلُّ ۖ وَما لَهُم مِن ناصِرينَ Hata ukiwa na pupa ya kutaka kuwaongoa, lakini Mwenyezi Mungu hamwongoi yule anaye shikilia kupotea. Wala hawatapata wa kuwanusuru.