19وَجاءَت سَيّارَةٌ فَأَرسَلوا وارِدَهُم فَأَدلىٰ دَلوَهُ ۖ قالَ يا بُشرىٰ هٰذا غُلامٌ ۚ وَأَسَرّوهُ بِضاعَةً ۚ وَاللَّهُ عَليمٌ بِما يَعمَلونَ Ukafika msafara, wakamtuma mchota maji wao, naye akatumbukiza ndoo yake. Alisema: Kheri Inshallah! Huyu hapa mvulana! Wakamficha ili kumfanya ni bidhaa. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa wanayo yatenda.