64لَهُمُ البُشرىٰ فِي الحَياةِ الدُّنيا وَفِي الآخِرَةِ ۚ لا تَبديلَ لِكَلِماتِ اللَّهِ ۚ ذٰلِكَ هُوَ الفَوزُ العَظيمُ Wao wana bishara njema katika maisha ya dunia na katika Akhera. Hapana mabadiliko katika maneno ya Mwenyezi Mungu. Huko ndiko kufuzu kukubwa.